Kuwashwa matakoni | na sehemu za siri

Hali ya kuwashwa matakoni

Hali ya mtu kuwashwa makalio na kujikuna sana husababishwa na mambo mbalimbali kama:-

Eczema

Huu ni ugonjwa wa allergy ya ngozi husababisha ngozi kuwa kavu na kuwasha, hivyo kama una shida hii makalio yanaweza kuwasha.

Lakini pia shida hii huwa inapelekea ngozi kuwasha sana na kupata vipele fulani.

Fangasi sehemu za siri

Unapokua na fangasi ya kwenye uke au kwenye korodani fangasi hao wanawazea kusambaa kwenye makalio na kusababisha muwasho

 

Kuvaa nguo zinazohifadhi joto

Unapovaa nguo za ndani ambazo ni nzito pamoja na nguo zinazohifadhi joto kama vile jeans na tracksuits zinapelekea jasho kujikusanya kwenye makalio na kusababisha muwasho.

Ugonjwa wa mashilingi

Hii ni aina fangasi inayosababisha vipele vinavyoota kama shilingi na kuwasha

Kuwa na michirizi kwenye makalio

Michirizi ya ngozi hutokana na ngozi kutanuka kupita kiasi hadi kuachia, inaweza kuwa na maumivu, michubuko pamoja na muwasho

Kuvaa nguo za kubana;

Nguo za ndani zinazobana sana kama vile chupi na skin tights hubana ngozi kupita kiasi na kusababisha muwasho Vile vile kua na maambukizi ya minyoo,au kua na bawasiri, kuharisha nk kunaweza kusababisha muwasho makalioni.

Matibabu yake hutegemea na chanzo cha tatizo kikubwa zingatia usafi wa sehemu za siri kwa kuhakikisha unajisafisha vizuri na pia kama tatizo litaendelea kwa muda mrefu inashauriwa kumuona Daktari kwa ajili ya vipimo na uchunguzi wa kina zaidi.

Msaada na Ushauri, Binafsi-wasiliana nasi Moja kwa moja kupitia namba.
0711 556 377
DR LUTAMBI

6 thoughts on “Kuwashwa matakoni | na sehemu za siri

  1. Forrest Robitaille Reply

    Unquestionably consider that which you said. Your favourite reason appeared to be at the internet the easiest factor to understand
    of. I say to you, I definitely get irked while other people think
    about concerns that they plainly don’t recognize about.
    You managed to hit the nail upon the highest and also outlined out the whole thing without having side
    effect , other folks can take a signal. Will likely be back to get more.
    Thanks

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *