Mambo 7 Ya Muhimu kuzingaria Kama unahitaji kushika Ujauzito
_____________________
Karibu sana katika makala hii tutaangazia zaidi suala tendo la ndoa na hatua mbalimbali zinavyoweza kuathiri uwezekano wako wa kushika mimba. Mambo gani mengine muhimu inayoyahitaji kama unahitaji kushika mimba.
Watu wengi kwa muda mrefu walikuwa wakijizuia kupata mimba lakini, kwa sasa ndo wanahitaji kushika mimba, lakimi wanashangaa, mimba hazinasi-wanabaki kujiuliza nini shida?.
Mambo muhimu ya kuzingatia Kama mnahitaji kushika mimba lakini Hazishiki.
1.-Fanya kipimo cha sperm analysis mwanaume ili ujiridhishe kuhusu ubora wa mbegu zako.
2.Kama Mzunguko wa hedhi wa mke upo sawa sawa-anapata kawaida kila mwezi.
Je! anapata ute wa Ovulation?
-Kama mambo hayapo sawa, ni Muhimu afanye Kipimo cha Ultrasound kuangalia mazingira ya uzazi, kama yapo safi-Na acheck Hormone profile kwa ajili ya Kuangalia-Kama hakuna shida ya Hormone imbalance.
NB:Ushauri ufuatao ni kwa wale ambao hawana shida Yoyote, kwa wote mwanaume na mwanamke.
*Tips Muhimu za kuzingatia*.
_*1.Fanya Mapenzi Kisawasawa.*_
Wengi kwa kujivungavunga wamajikuta wanapishana na Siku rasmi za kupata watoto.
Tendo la ndoa, ni tendo jema kwa wanandoa, Ni haki ya kila mwana ndoa kulifurahia, na kushukuru kwa upatikanaji wake. Kama mume wako anaitisha mara kwa mara, mpe ale ashibe. Kama Hakuna maelewano, malizeni changamoti zenu mapema-ili ndoa iendelee.
Kama munatafuta watoto-Siku za kuruka ni siku za hedhi tu. baada ya hapo Ni Furaha mpaka mwisho wa mwezi.wastani wa chini ni Mara 3 kwa wiki.
_*2.Kama Mzunguko ni Linganifu na Haubadiliki badiliki-Kusudia Kushiriki tendo ndani ya Siku za hatari. (Ovulation window)*_
Jitahidi ujue siku ya ovulation itakuw lini, na ufanye mapenzi siku 1 kabla ya ovulation au katika siku Husika ya Ovulation.
Japo hata ukifanya Siku 2-Kabla ya ovulation uwezekano wa kushika mimba upo sawa hasa kama mwanaume anatoa mbegu Bora.
Mbegu z mwanaume zinaweza kuishi hadi siku 3, Katika mfumo wa uzazi wa mwanamke bila kuharibika.
Lakini yai la uzazi (Yai la mwanamke) Linaishi ndani ya masaa 24 tu, baada ya hapo kama halijarutubishwa linaharibika.
Unaweza kujua siku ya Ovulation kwa Njia ya Kuhesabu mzunguko wako wa hedhi au kwa kutumia Ovulation kit.
Kama mzunguko wako wa hedhi upo kawaida.
Siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi.ni ile unayoanza kuona damu ya hedhi.Na siku ya mwisho ni ile siku moja kabla ya kuanza kuona tena damu kwa awamu inayofuata.
_*3.Fuatilia urefu wa Mzunguko wako.*_
Fuatilia Miezi 2-3 ili kujiridhisha kama mzunguko wako haubadiliki badiliki-Na kama haubadiliki-ujue urefu wake ni siku ngapi? (28 ni wastani-Lakini Kuna mzunguko mfupi (21-26 na Mrefu 30-35).Kujua mzunguko wako itakusaidia sana katika kushika Mimba. Maana siju za ovulation zinabadilika kulingana na urefu wa mzunguko wako.
Kama mzunguko ni siku 28-Automatically Ovulation inakuwa siku ya 13-14.
Kwa hiyo hapo unaweza kuanza kushiriki siku ya 11- Hadi 14
_*4.Tumia Ovulation Predictor Kit Ili Kurahisisha Jambo.*_
Ovulation strip (Ovulation kit) ni Vifaa vinavyopima Homoni ya LH (Lutenizing Hormone) katika mkojo.Lutenizing huwa nyingi katika siku ya Ovulation.
Kipimo kikichola mistari Miwili iliyokoza-Ujue masaa machache toka muda huo-upo kwenye ovulation. Huo ndo muda mzuri wa kutekeleza Tukio la kupanda mbegu kwa njia ya tendo la ndoa.Tena Huu ni Muda mwafaka sana kwa wanohitaji mtoto wa kiume.
_*5.Pima Joto La Asubuhi*_.
Kwa kupima Joto la Asubuhi la kinywani kila asubuhi-Husaidia kujua Siku ya ovulation ni Ipi?
Siku ya Ovulation Joto huwa juu kidogo-utadhani upo na Homa.
Joto la asubuhi-hutakiwa kupimwa,Mara baada ya kuamka-kabla hata hujapika mswaki.
_*6.Angalia Ute wa Ovulation (Cervical Mucus).*_
Ukitoka kwenye hedhi kuna uchafu utatoka kidogo, baadae utaongezeka, baadae utaongezeka zaidi.Ute wa ovulation ni mzito kama ute mweupe wa yai-unavutika vutika kama ute wa yai. Ukiona hiyo-hakuna kuuliza upo kwenye siku ya Ovulation.Huo ndo muda mzuri sana wa Kushiriki tendo la ndoa.
Kufanya mapenzi siku moja kabla ya ovulation au katika siku ya ovulation, ni shabaha nzuri sana kwa ajili ya kushika mimba.
_*7.Mwanamke Usikurupuke kuamka Mara baada ya tendo.*_
Ukimaliza tendo tumia Muda mrefu kidogo kubakia kitandani (Dakika 20-30 zinatosha), ukiwa umejilaza. tumia muda huo kupiga story au Kuchapa usingizi (inategemeana na kazi yenu ipoje).
Kukaa hapo kwa muda kunasaidia mbegu za uzazi za mwanaume kusafiri kwa kasi kuelekea yai la uzazi-Hivyo kutengeneza uwezekano mkubwa wa mbegu Kufika kwenye yai mapem na kufanya urutubishaji.
*Mambo ya Kuepuka:*
▪️-Usinye kitu cha baridi sana baadavya tendo la ndoa.Maji,soda n.k
▪️-Usinywe kinywaji chochote chenye kafeini (kahawa,chai,energy drink, soda nyeusi n.k)
Hizi zinaharibu sana mbegu za uzazi za mwanaume.
▪️-Usitumie kabisa Vilainishi vya kisasa wakati wa tendo l ndoa (artificial sexual lubricants).
▪️-Kama kutakuwa na ulazima wa kuamka kwa ajili yabkwendavkukojoa-Nenda mara moja kojoa-kishabrudi ujilaze.
Kukojoa mara baada ya tendo la ndoa husaidia kupunguza hatari ya kupata U.T.I
*Zingatia:* Natural Lubrication ipo ndani ya mwanamke mwenyewe-Zingatia kufanya Mchezo mrefu, kabla ya tendo ili kufanya Atoe maji mengi n kuwa mlaini wakati wa Tendo.Pia bado utakuwa unaendwlea kuwezesha mbegu kuogelea vema kuelekea kwenye mirija ya fallopia ili kukutana na yai.
Kama unahitaji kushika mimba na unahitaji kushikwa mkono kwa msaada wa dakitari kufikia azima hiyo-Usikose kuwasiliana nasi-Tumia namba 0745 889 503 wasiliana nasi kwa Simu au WhatsApp.
Kama Unakabiliwa na mvurugiko wa homoni-Hedhi zako zinavurugika vurugika-Tutakupatia dawa ya kurudisha mpangilio wako kwa haraka,Kisha utakuwa na uwezo wa kushika mimba kwa urahisi.
You’ve made some deecent points there. I checked
on the web for more information aout the issue and found most individuals will go along with your views on this website. https://lvivforum.Pp.ua/