Mimba ikitoka ukae Muda gani Kushika tena?

*MIMBA IKIPOROMOKA KWA BAHATI MBAYA (MISCARRIAGE) UKAE MUDA GANI KUSHIKA TENA?*
________________

Wengi ambao hupoteza Ujauzito kwa bahati mbaya hujikuta wakijaribu kushika mimba katika siku chache zijazo, Jambo hili siyo tu kwamba halifai-pia ni hatari.

Hapa tutazungumzia nini kifanyike, katika mizunguko inayofuata.

Mimba kuporomoka ni jambo ambalo linawatokea wanawake wengi sana-lakini Jambo hili halizungumzwi sana-Hivyo wengi wanakuwa gizani nakujikuta wakifanya makosa yale yale na kuhatarisha afya zao.

Mimba kuporomoka ni changamoto kubwa zaidi-inakadiriwa kuwa mimba 1 kati ya 4 zilizotungwa huishia kwenye kuharibika (25%). Baadhi wakiwa wanaharibikiwa hata bila kujua kama walikuwa na mimba.

Baada ya mimba kuharibika unashauriwa kukaa miezi shida ndipo ushike ujauzito mwingine.

1. Kama Hiyo ni mara yako ya kwanza mimba kuporomoka:
– Unaweza kushika ujauzito mwingine mara tu baada ya kuendelea kupata siku zako za hedhi. (wastani baada ya wiki 6 tangu ujauzito wako kuharibika).
– Hii inategemea afya yako . Lakini usishike mimba katika muda huo kabla ya miezi 6. kwa sababu itaongeza hatari ya mimba kuendelea kutoka.

2. Kama umewahi kutoa mimba hapo awali:
– Unashauriwa Zaidi kusubiri mpaka miezi 6 ikamilike. hii itakuepushia hatari ya kupata makovu kwenye kizazi. Hali inayoweza kupelekea kupata utasa (kupoteza kabisa uwezo wa kushika mimba).

Kumbuka
– Baada ya mimba kutoka, “hormoni za mimba (HCG)” zinaweza kuwepo Mwilini kwa muda fulani, na hivyo kupelekea hali ya kuchelewa kwa siku za hedhi kurudi kawaida.
– Ikiwa baada ya miezi miwili utakuwa bado hujapata hedhi, unaweza kufanya tena kipimo cha mkojo kuona kama kuna mimba au ni changamoto ya mvurugiko wa homoni ndo inaendelea.

*SABABU ZA MIMBA KUHARIBIKA NI HIZI*.
Sababu nyingi hupelekea mimba kuporomoka lakini miongoni mwa sababu inayoqapata wengi ni ile tunayoiita Aneuploidy.

Aneuploid Ni shida ya kuwa na namba ya chromosome zisizo za kawaida (abnormal chromosome number).

Hali hii huongezeka kadri umri unavyoongezeka.Kwa vile wanawake huzaliwa na mayai yao yakiwapo tayari katika ovary.Unapozaliwa yanakuwa yamechaguliwa kwa ajili ya kutolewa (ovulation) katika vipindi tofauti vya maisha yako.

Kwa hiyo mayai mengi yanakuwepo pale yamesubiri zamu ifike kwa muda wa miaka mingi. Protein zake huharibika na chromosome kukaa kwenye mkao usiyotakiwa.Mara nyingi Zinapungua zinakuwa chini ya 23.

Mimba inapotungwa inakuwa na chromosome 46.
Chromosome 23-kutoka kwa yai za mama.

na Chromosome 23-Kutoka katika Mbegu ya Baba.Hizi chromosome ni seti za Kigenetiki ambazo zinahitajika kwa ajili ya Kurithisha tabia za wazazi kuja kwa mtoto.

Yai lenye Chromosome pungufu-ya 23.Mimba ikitungwa mara nyingi huishia kuharibika. Ndo maana kuharibika kwa mimba huongezeka kadri umri unavyoongezeka.

Kuanzia miaka 40 kwenda juu, Kasi ya mimva kuharibika huongezeka zaidi kabla ya muda huo.ukilata mimba Katika umri wa 40+ Uwezekano wa mimba kuharibika ni 40%-Hii inatokana na kuharibika kwa mpangilio wa Chromosomes.

Sababu zingine za Mimba kuporomoka ni Pamoja na:
Mvurugiko wa Hormone za Endocrine, yakiwemo magonjwa ya tezi ya shingo.

Kupungukiwa Hormone zinazozalishwa na tezi ya shingo (Thyroidine deprivation)-Ni miongoni mwa sababu kubwa inayopelekea mimba nyingi sna kuharibika.

Lakini baadhi Mimba huharibika kwa sababu ya Magonjwa ya autoimmune ambapo unakuwa na Antiphospholipid Antibody syndrome-ambayo husababisha kuganda kwa damu,Katika kizazi na mimba huharibika kw urahisi.

Lakini wengi zaidi mimba huharibika kutokna n kuwepo kwa Maambukizi ya P.I.D Katika kizazi. wengi sana wameshindwa kushika mimba kwa sababu hii, na baadhi mimba hupolomoka mapema zaidi hata kabla ya kujua kama wanaujauzito.

Sababu nyingine ni Kulegea kwa Mlango wa kizazi (Cervical Incompetence).
shingo ya kizazi inapokuwa dhaifu, mimba inapojishikiza kwenye kizazi, huwa haiwezi kustahimiri kqa muda mrefu.

Kutoka kwenye Sababu zilizooneshwa hapo juu,changamoto yako yako inaweza kutokana na sababu fulani, Unapaswa kufanya vipimo kwa ajili ya Kudhibitisha.Kisha kupata matibabu Kulingana na Hali yako inayosabbisha.

Sababu nyingi kati ya hizo zinaweza kurekebishwa,Na ukarudi kwenye hali yako ya kawaida, na ukaweza kushika mimba Kama kawaida.

Kama unahitaji msaada wa kuzuia changamoto za mimba kutoka, Unaweza kutubiwa kwanza kwenye chanzo cha tatizo lako na mambo yatakwenda vizuri zaidi.

Fika kituoni kwetu Dar es salaam.Kwa ajili ya Msaada wa matibabu,Au wasilina nasi Moja kwa moja, 0745 889 503 Piga simu Au WhatsApp

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *