bawasiri

Ugonjwa wa Bawasiri | Mambo 5 Unayopaswa kuyafahamu.

1.Ugonjwa wa Bawasiri Ni nini?

Bawasiri au Kwa kiingereza ni hemorrhoids ni hali inayotokea kama kinyama kwenye njiaya haja kubwa. Hii hutokea wakati ambapo mishipa inayozunguka eneo la puru au njia ya haja kubwa inakuwa yenye
na kisha kuvimba, kulegea, na kusababisha maumivu au usumbufu zaidi.

Kuna aina mbili za bawasiri: bawasiri za nje ambazo zinapatikana nje ya eneo la puru na bawasiri za ndani ambazo zinapatikana ndani ya njia ya haja kubwa.

2.Dalili za bawasiri Ni zipi?

dalili-za-bawasiri

Soma pia: Ili kupona vidonda vya tumbo-Suluhisho bora ni hili Hapa.

Mtu mwenye ugonjwa wa bawasiri anaweza kuwa na dalili zifuatazo:
1.Kutokwa na kinyama katika njia ya haja kubwa
2.Kupata Maumivu au usumbufu katika eneo la puru au njia ya haja kubwa.
3.Kuwashwa au kuhisi kama kuna kuchomwa katika eneo hilo la haja kubwa.
4.Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa.
5.Kuhisi una kitu kigumu kimekwama katika puru au njia ya haja kubwa.
6.Kupata Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa.

  1. Kupata maumivu wakati wa kukaa mara baada ya kujisaidia haja kubwa.
  2. Hisia ya kutokwa na kitu kinachoshikamana na njia ya haja kubwa baada ya kupata choo.

Ukiwa na moja au baadhi ya dalili hizo, ni wakati wa kuwasiliana na dakitari ili kupata mwongozo mapema wa jinsi ya kuondokana kabisa na shida hiyo.

sababu-za-bawasiri

Soma pia: Maumivu ya tumbo la hedhi (Dysmenorrhoea | chango la uzazi

3.sababu za bawasiri ni Hizi hapa.

Bawasiri ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kumpata mtu yeyote, lakini kwa kiasi kikubwa inahusishwa na tabia na mienendo fulani ya kila siku.
Sababu za kuchangia ugonjwa wa bawasiri zinaweza kuwa kama ifuatavyo:

  1. Kujisukuma kwa nguvu wakati wa kujisaidia haja kubwa: Hatua ya kujisaidia haja kubwa inaweza kuwa sababu kubwa ya kuibuka kwa tatizo hili.
    Kujisukuma kwa nguvu sana wakati wa kujisaidia husababisha shinikizo kubwa kwenye mishipa ya damu inayozunguka eneo la puru (mkundu), na hivyo
    kusababisha mishipa hiyo kutanuka au kupanuka na kisha kutokea kwa ugonjwa huu wa hemorrhoid.
  2. Kukaa kwa muda mrefu: Kama unafanya kazi za Kukaa kwa muda mrefu, upo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo hili. watu kama madereva wa maroli, mafundi cherehani, wafanya kazi wa ofisini wanaokaa muda mrefu n.k wapo hatarini zaidi, hasa kama wanatumia vyakula vilivyokobolewa.
    Pia hata kukaa kwa muda mrefu kwenye choo kunaweza kuleta shinikizo kwenye mishipa ya damu katika eneo la puru na njia ya haja kubwa.
    Hii inaweza kusababisha mishipa hiyo kukandamizwa na kusababisha tatizo hili kutokea.
  3. Unene kupita kiasi: Watu wanene na walio na uzito mkubwa wapo hatarini zaidi kupata bawasiri kuliko watu wa kawaida.
    Unene husababisha shinikizo kubwa kwenye mishipa ya damu, hususani kwenye eneo la puru na njia ya haja kubwa.
    Unene huongeza hatari ya kutokea kwa bawasiri kwa sababu ya shinikizo hili, ambalo hupelekea mishipa ya damu kutuna.
  4. Kuwa na Ujauzito: Wanawake wengi hupata zaidi bawasiri wakiwa kwenye hali ya ujauzito. Wanawake wajawazito wanaweza kuwa na hatari kubwa ya kupata bawasiri kutokana na shinikizo linalozidi kwenye eneo hilo la puru wakati wa ujauzito.
    Uzito wa ujauzito unaweza kuongeza shinikizo kwenye mishipa ya damu karibu na sehemu ya puru na hiyo ndiyo sababu wajawazito wengi hujikuta wanapata bawasiri.
  5. Kupata choo kigumu mara kwa mara (constipation): Choo kigumu kwa vile kinakufanya uwe unajisukuma kwa nguvu wakati wa kujisaidia haja kubwa.
    Hii inaweza kusababisha mishipa ya damu kusumbuka, kutuna na hata kupasuka na kusababisha bawasiri ijitokeze.
  6. Kupata maambukizi ya mara kwa mara katika eneo la puru: Maambukizi ya mara kwa mara katika eneo la puru yanaweza kusababisha kupanuka kwa mishipa ya damu kwenye eneo hilo, na hivyo kusababisha bawasiri.
tiba-ya-bawasiri-1

Soma pia: Fahamu kila kitu kuhusu Kiungulia | Mambo 5 Muhimu.

4.Tiba ya bawasiri Ipoje?

Tiba ya bawasiri inategemea ukali wa hali ya bawasiri ilivyo muda huo na dalili zinazojitokeza zipoje. Hapa kuna baadhi ya njia za tiba za bawasiri ambazo hutumika sana:

  • Kubadili Mtindo wa Maisha: Kwa bawasiri ambazo ni za hali ya chini na zisizo na matatizo makubwa, mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kuwa tiba ya tosha. Hii inaweza kujumuisha kuepuka kujisukuma kwa nguvu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuhakikisha unakula vyakula vyenye nyuzi nyingi na kupata maji ya kutosha, kufanya mazoezi na pia kupunguza unene kupita kiasi.
  • Matumizi ya Dawa : Hapa kuna Dawa za kupaka na dawa za vidonge ambazo hutumika sana katika matibabu. Baadhi zinaweza kutumiwa kupunguza maumivu, kuondoa uvimbe wa mishipa ya damu, na kupunguza uvujaji wa damu kwa wagonjwa wenye bawasiri.
  • Daktari ataweza kupendekeza dawa husika kulingana na hali ya mgonjwa ilivyo.
  • Tiba ya Sklerotherapia (Sclerotherapy): Hii ni njia ya matibabu ambayo inaweza kutumika kutibu bawasiri zilizopo ndani ya puru kwa kuingiza kitu maalum ndani ya bawasiri, huifyonza mishipa iliyotuna na hatimaye kunywea na kupungua.
  • Tiba ya Ligation (Hemorrhoid Ligation): Hii ni njia ya upasuaji ambayo inahusisha kuifunga mishipa iliyosababisha bawasiri ili kuzuia damu kuingia katika mishipa hiyo na hivyo kupunguza ukubwa wa bawasiri, kwa sababu damu inakuwa imezuiwa kuingia kwenye mishipa hiyo, ndo maana vinyama vilivyovimba vinanywea.
  • Kufanyiwa Upasuaji: Kwa hali za kawaida sana au za hali ya juu, upasuaji unaweza kuwa chaguo la tiba, kwa tatizo lililoshindikana.
  • Upasuaji unaweza kufanyika kwa njia ya kawaida au kwa njia ya laparoscopic (upasuaji wa matundu madogo madogo), Upasuaji hufanyika kulingana na hali ya mgonjwa ilivyo.
  • Kutumia Dawa Asilia: Kuna mimea na viungo vya asilia ambavyo vinaweza kutumika kama tiba ya bawasiri. Mimea kama aloe vera, chamomile, witch hazel, na mafuta ya nazi vinaaminika kusaidia kupunguza maumivu, kuvimba, na kusaidia kuponya bawasiri.
  • Pia, kula vyakula vyenye viungo vya asili kama vitunguu swaumu, tangawizi, na mboga za kijani zinaaminika kuwa na faida katika kupunguza dalili za bawasiri.
jinsi-ya-kujikinga-na-bawasiri

Soma pia: P.I.D Ni nini? | Dalili, Sababu na Matibabu.

5.Jinsi Gani ya kujikinga na bawasiri

Kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua ili kujikinga na bawasiri au kupunguza hatari ya kuzipata bawasiri:

  1. Hakikisha Unakula Lishe Bora: Kula vyakula vyenye nyuzi nyingi kama matunda, mboga, nafaka nzima, na mboga za kijani. Lishe bora inaweza kusaidia kuzuia kufunga choo na hivyo kupunguza hatari ya kujenga shinikizo kubwa kwenye puru.
  2. Kunywa Maji Mengi: Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku inaweza kusaidia kudumisha unyevunyevu wa kutosha mwilini na kufanya mchakato wa kujisaidia haja kubwa uwe rahisi zaidi.
  3. Zingatia Kufanya Mazoezi: Kufanya mazoezi mara kwa mara kunaweza kusaidia kudumisha uzito wa mwili unaofaa na kuzuia hali ya kufunga choo (constipation).
  4. Epuka Kusukuma sana Wakati wa Kujisaidia: Kusukuma wakati wa kujisaidia haja kubwa kunaweza kuongeza shinikizo kwenye puru na kusababisha ugonjwa huu. Epuka kusukuma sana mapema badala yake unapaswa usubiri hadi haja ikishaanza kutoka vizuri.
  5. Usikae kwenye choo kwa muda mrefu: Hasa vyoo vya kukali. Kukaa kwa muda mrefu kwenye choo kuongeza shinikizo kwenye puru. Jaribu kufanya shughuli ya kujisaidia iwe ya muda mfupi.
  6. Jisafishe vizuri Baada ya Kujisaidia: Hii ni njia moja ya kukinga maambukizi kwenye eneo la puru ambayo inaweza kusababisha kupata tatizo hili, hakikisha unatawaza vizuri na kujikausha uwe safi.

Kwa kufuata hatua hizi za kujikinga na ugonjwa huu, unaweza kupunguza hatari ya kuwapata na kuhakikisha afya bora ya puru na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa ujumla wake.

 

Kupata Tiba ya Kumaliza kabisa tatizo la bawasiri wasiliana nasi WhatsApp au normal call kwa namba 0745 889 503. Kila la Heri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *