Changamoto za-p.i.d

ugonjwa wa p i d, Sababu na Tiba yake | Njia 6 za Kuzuia.

ugonjwa wa p i d Ni nini?

Huu ni Ugonjwa wa maambukizi kwenye kizazi Unaotokea kwa wanawake.

PID ni kifupi cha “Pelvic Inflammatory Disease” ambayo ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke Inaweza kuhusisha shingo ya kizazi, mji wa mimba (kizazi-uterus) mirija ya uzazi, ovari, na sehemu nyingine za mfumo wa uzazi.


ugonjwa wa p i d ambao ni maambukizi ya viungo vya uzazi (PID) hutokea kwenye sehemu moja au zaidi ya viungo kadhaa vya uzazi katika sehemu za juu za kizazi, sehemu hizo ni pamoja na shingo ya kizazi (cervix) kizazi au mji wa mimba (uterus), mirija ya uzazi pamoja na ovari.


ugonjwa wa p i d ukiachwa bila kutibiwa unaweza kusababisha kutokea kwa makovu ndani ya mirija ya uzazi, pia mirija inaweza kujaa maji , na kuwa na majipu (absess).
Inaweza kuathiri karibu kila sehemu ya kwenye mfumo wa uzazi, ambayo inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu, unaoweza kupelekea kushindwa kabisa kushika mimba (utasa).

Soma Pia: A-Z Kuhusu Ugonjwa wa kisukari | Sababu, na Dalili zake

Dalili za ugonjwa wa p i d (maambukizi kwenye kizazi) zinaweza kuwa za kawaida au kali zaidii.
Baadhi ya wanawake huwa hawapati dalili zozote nzito. Ikitokea hivyo , huenda usigundue una ugonjwa huo mpaka unapoanza kupata shida ya kutunga mimba (kubeba ujauzito) au
pale unapoendelea kuwa na maumivu ya mara kwa mara kwenye eneo la kizazi (tumboni chini ya kitovu).

dalili ya p.i.d

p.i.d dalili zake ni rahisi kuzitofautisha na magonjwa mengine. Japo kuna wakati Dalili za ugonjwa wa p i d au Maambukizi katika kizazi zinaweza kuwa za kawaida tu au ngumu kuzitambua.
Lakini mara nyingi huwa ni za waziwazi, japo Baadhi ya wanawake wanaweza kutoonesha dalili zozote kabisa.
Lakini pale dalili za ugonjwa wa kizazi (PID) zinapojitokeza, zinaweza kujumuisha zifuatazo:

  • Mwanamke juhisi Maumivu ya tumbo chini ya kitovu— Hutokea mwanzo zikiwa dhaifu baadae zinakuwa kali zaidi —zingatia kuwa hutokea kwenye tumbo la chini ya kitovu hadi kwenye nyonga, hayo ndiyo maeneo ya viungo vya kizazi vya ndani yalipo.
  • Kutokwa na uchafu ukeni. Uchafu usio wa kawaida, unaweza kuwa mwingi ambao unaweza kuwa na harufu mbaya sana. Mara nyingi unakuwa kama maziwa mgando.
  • Kutokwa damu ukeni. Kuvuja damu kusivyo kawaida kutoka ukeni, hususani wakati wa tendo la ndoa au mara baada ya tendo la ndoa, au kati kati ya vipindi vya hedhi, ni dalili mbaya zaidi ya P.I.D.

Soma Pia: Maumivu ya tumbo la hedhi (Dysmenorrhoea | chango la uzazi

  • Maumivu wakati wa tendo la Ndoa. Unapofanya tendo la ndoa unahisi maumivu makali sana, mwanaume akiingiza ndani unahisi kuna kitu anakigusa, unatamani kuchomoa, hiyo ni kiashiria cha wazi upo na maambukizi katika kizazi, yanayojulikana kama ugonjwa wa p i d
  • Homa kali za mara kwa mara, mara nyingine zinaambatana pamoja na kutetemeka. Hali hii inakuwa na joto kali la mwili. Kupandisha Homa, na joto la mwili likizidi 101 F (38.3 C).

Muda sahihi wa kuonana na Dakitari.

Tafuta mtoa huduma wa afya au kutafuta matibabu ya haraka ikiwa unaona moja wapo ya mambo yafuatayo:

  • unapopata Maumivu makali chini ya tumbo (chini ya kitovu)
  • Unapohisi Kichefuchefu na kutapika, hata usiweze kukaa na kitu tumboni, yaani unatapika sana.
  • Kupandisha Homa, na joto la mwili likizidi 101 F (38.3 C), mwone dakitari kwa haraka.
  • Unapotokwa na uchafu ukeni. ukitokwa uchafu ukeni wenye harufu mbaya, mwone dakitari mara moja.

Zingatia kuwa Ikiwa una dalili za ugonjwa wa p i d ambazo si kali, usipuuze muone mtoa huduma wa afya kwa haraka iwezekanavyo.

Miongone mwa hizo ni Hizi: Kutokwa uchafu ukeni, uchafu wenye harufu mbaya, Unapata maumivu wakati wa kukojoa au unaona kutokwa na damu kati ya vipindi vya hedhi, unapata maumivu wakati wa kujamiana (wakati wa tendo la ndoa) zote hiz ni dalili za wazi za uwepo wa maambukizo ya magonjwa yanayoendezwa kwa njia ya zinaa (kujamiana).


Ikiwa dalili hizi zinatokea, acha kujamiana kwa muda mpaka utakapopona na muone mtoa huduma ya afya haraka.
Matibabu ya haraka ya maambukizo ya zinaa yanaweza kusaidia kuzuia PID.

Zingatia hili ukiwa na Dalili za P.I.D
p.i.d-husababishwa-na-nini

Soma pia: Ili kupona vidonda vya tumbo-Suluhisho bora ni hili Hapa.

P.i.d husababishwa na nini

Sababu za Ugonjwa wa P.I.D

  • Maambukizi ya Magonjwa ya zinaa:

Aina nyingi za bakteria zinaweza kusababisha PID, lakini maambukizo ya kisonono au klamidia ndio yanayotokea sana na kusababisha ugonjwa huu.
Bakteria hawa kwa kawaida hupatikana wakati wa tendo la ndoa bila kinga. Kwa hiyo wazinzi wanakuwa kwenye hatari zaidi ya kupokea ugonjwa huu na kuusambaza.

  • Kubadilika kwa Hali ya pH ya ukeni:

Kwa nyakati fulani bakteria wanaweza kuingia kwenye kizazi wakati kizuizi cha kawaida kilichopo kwenye mlango wa kizazi kinapoharibiwa.
Kwa mfano: Hali Hii inaweza kutokea wakati wa hedhi na baada ya mwanamke kujifungua, au pale mimba inapokuwa imeharibika au kuporomoka, PH ya uke, hubadilika kidogo, kwa hiyo inaweza kuwa rahisi kwa bakiteria kupenya kutoka ukeni, na kuingia kwenye kizazi.

  • Kutumia kitanzi kama njia ya uzazi wa mpango:

Japo Kwa nadra, bakteria wanaweza pia kuingia kwenye kizazi wakati wa kuiwekewa kitanzi (kifaa cha uzazi wa mpango (IUD) – aina ya njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu – au unapofanyiwa taratibu yoyote ya matibabu inayohusisha kuingiza vifaa kwenye mfuko wa uzazi, maambukizi yanaweza kutokea.

Watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata P.I.D

Sababu Hatarishi za Ugonjwa wa PID
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kuongeza hatari yako ya kupata ugonjwa wa Maambukizi kwenye mfuko wa uzazi, ikiwa ni pamoja na:

  • Kushiriki tendo la ndoa na watu ukiwa na umri chini ya miaka 25
  • Kuwa na wapenzi wengi.
  • Kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye ana wapenzi wengi (wapenzi zaidi ya mmoja)
  • Kufanya ngono bila kutumia kinga.
  • Kuosha na maji ukeni mara kwa mara, ambayo inachanganya uwiano wa bakteria wema na wabaya katika uke na inaweza, kufanya katizo lako lisipone kwa haraka.
  • Kuwa na historia ya ugonjwa wa PID Au magonjwa mengine ya zinaa.
  • Kuwekewa kipandikizi: Japo Kuna hatari ndogo ya kuambukizwa PID baada ya kuingizwa kwa kifaa cha uzazi wa mpango cha kitanzi (IUD). Hatari hii kwa ujumla inahusiana na wiki tatu za kwanza baada ya kuingizwa, zaidi ya hapo labda upate kwa njia nyingine.

Soma pia: mvurugiko wa homoni | Tatizo la Hyperprolactinemia

Madhara ya p.i.d

Madhara na Changamoto za Ugonjwa wa PID.

Ugonjwa wa p.i.d husababisha madhara mbalimbali kwa mwanamke, kusababisha tishu za uzazi kupata makovu na kujaa maji na kuwa na majipu (abscesses) huweza kutokea katika mfumo wa uzazi.
Changamoto Hizi zinaweza kusababisha uharibifu wa kudumu kwa viungo vya uzazi vya mwanamke, na kumweka kwenye wakati mgumu zaidi wa kushika mimba.

Matatizo au madhra yanayotokana na uharibifu huu yanaweza kujumuisha:

1.Mimba kutunga nje ya kizazi:

PID ni sababu kuu ya mimba kutunga nje ya kizazi (ectopic pregnancy) Hii ni hali ambayo mimba hujipandikaza katika mirija ya uzazi, au nje ya hapo, tofauti kabisa na eneo rasmi la mimba kujipandikiza ambalo ni kwenye kizazi (uterus).


Mimba iliyotungwa nje ya kizazi inaweza kutokea wakati PID ambayo haikutibiwa inapokuwa imesababisha makovu kutokea katika mirija ya fallopian (mirija ya uzazi).
Tishu hizo za makovu zinazuia yai ambalo halijarutubishwa kupita kwenye mirija ya fallopian na kuweza kujiweka katika mfuko wa kizazi.
Badala yake, yai huanza kujiweka katika mirija ya fallopian.

Mimba iliyotungwa nje ya mji wa mimba (uterus) inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi inayoweza kusababisha hatari ya kupoteza maisha na hivyo huhitaji matibabu ya dharura.

2.Kupata shida ya kushika Mimba na utasa:

Uharibifu kwa viungo vyako vya uzazi unaweza kusababisha ugumba (ukosefu wa uzazi) -Hali inayofanya kutokuwa na uwezo wa kupata ujauzito.
Kadiri unavyoendelea kupata PID, ndivyo hatari yako ya kuwa tasa inavyoongezeka. Pia Kuchelewesha matibabu ya PID ndiyo huongeza kwa kiwango kikubwa zaidi hatari ya kukosa uzazi.

3.Kuwa na Maumivu sugu katika Nyonga (Eneo la kizazi):


Maumivu ya mara kwa mara katika eneo la nyonga (pelvic) hutokea kama matokeo ya kawaida kwa watu waliopata Ugonjwa p.i.d, na wakachelewa kutibiwa au wametibiwa bila kupona.

Ugonjwa Huu wa maambukizi kwenye kizazi unaweza kusababisha maumivu makali sana ya pelvic (nyonga) ambayo yanaweza kudumu kwa miezi au miaka.

4.Maumivu wakati wa tendo la ndoa:


Makovu katika mirija yako ya fallopian na viungo vingine vya uzazi katika nyonga vinaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na wakati wa ovulation.

5.Majipu katika Mirija ya uzazi na Fuko la mayai (Tubo-ovarian abscess):

Changamoto za-p.i.d

Soma pia: Fahamu kila kitu kuhusu Kiungulia | Mambo 5 Muhimu.


PID inaweza kusababisha kuwa na uvimbe wa majipu (abscess) -ambao ni mkusanyiko wa usaha – kutokea katika mfumo wako wa uzazi. kwa Kawaida, huu uvimbe (abscess) husababisha mirija ya fallopian na ovari kudhurika vibaya sana,
lakini pia vimbe zinaweza kukuwa katika mfuko wa kizazi au viungo vingine vya uzazi katika nyonga (pelvic organs).
Ikiwa vimbe hizi (abscess) hazitatibiwa, unaweza kupata maambukizi hatari zaidi ya kuhatarisha maisha.

Antibiotic za kutibu pid

antibiotic Zinazotumika za kutibu pid
Kuna aina mbalimbali za antibiotic ambazo hutumiwa katika matibabu ya Pelvic Inflammatory Disease (PID).
Matibabu ya PID yanahusisha kutumia antibiotic kwa muda ili kuangamiza bakteria au vimelea vinavyosababisha maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.

Baadhi ya antibiotic ambazo mara nyingi hutumiwa katika matibabu ya PID ni pamoja na doxycycline, metronidazole, ceftriaxone, na azithromycin.
Kwa kawaida, daktari ataamua aina ya antibiotic na muda wa matibabu kutegemeana na aina ya bakteria au maambukizi yanayosababisha PID, pamoja na hali ya mgonjwa na viashiria vya ugonjwa.

Ni muhimu kumaliza dozi zako za antibiotic kama ilivyopendekezwa na daktari hata hata kama dalili za ugonjwa zinaisha mapema ili kuhakikisha kuwa maambukizi yameangamizwa kabisa.
Kukamilisha matibabu yote ni muhimu kwa kuzuia ugonjwa kurudi tena au kuenea kwenye viungo vingine vya uzazi.

Pia, ni vyema kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na daktari wako baada ya kutumia antibiotic ili kuhakikisha kuwa maambukizi yamepona kabisa na kuepuka matatizo ya muda mrefu yanayoweza kusababishwa na PID.
Kama una maswali au wasiwasi wowote kuhusu matibabu yako, usisite kuzungumza na daktari wako.

Njia za Kuzuia Ugonjwa wa P.I.D

Njia za ambazo huweza kutumika Kuzuia Ugonjwa wa P.I.D
Ili kupunguza hatari yako ya kupata ugonjwa wa Maambukizi katika kizazi, hakikisha unazingatia mambo haya:

Soma pia: vidonda vya tumbo Mambo 5 Muhimu sana Kuyajua.

1.Shiriki ngono salama:
Tumia kondomu kila unaposhiriki tendo la ndoa, punguza idadi ya wapenzi wako na uliza kuhusu historia ya ngono ya mpenzi wako, bahati mbaya sana kwako ikiwa atakudanganya.

2.Chagua njia Bora ya uzazi wa mpango:
zungumza na mtoaji wako wa huduma ya afya kuhusu uzazi wa mpango. Aina nyingi za uzazi wa mpango hazilindi dhidi ya kuenea kwa huu ugonjwa wa maambukizi kwenye kizazi.
Kutumia njia za kizuizi, kama vile kondomu, husaidia kupunguza hatari yako, kupata maambukizi haya.

Hata kama unatumia vidonge vya uzazi wa mpango, tumia kondomu kila unapofanya tendo la ndoa na mpenzi mpya ili kujilinda dhidi ya maambukizi ya zinaa.

3.Fanya vipimo :
Ikiwa uko katika hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa, fanya miadi na mtoaji huduma wa huduma ya afya kwa ajili ya kufanya vipimo.
Weka ratiba ya mara kwa mara ya upimaji kila inakuwa ikihitajika.

4.Pata Matibabu mapema:
ukiwa na dalili tu hakikisha unapata tiba ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa ili kukupa nafasi bora ya kuepuka ugonjwa wa maambukizi kwenye kizazi (PID).

5.Pima pamoja na mwenzi wako:
Taka mshirika wako apimwe. Ikiwa una ugonjwa wamaambukizi kwenye kizazi, shauri mshirika wako apimwe na atibiwe, pia ili asije akarudi kupandikiza maambukizi kwako, hata baada ya kuwa umepona.

Hii inaweza kuzuia kuenea kwa maambukizi zaidi katika kizazi na kurudi kwa ugonjwa wa maambukizi katika kizazi (PID).

6.Epuka kujichokonoa mara kwa mara:

  • usiwe unaosha uke kila mara kwa mara,Usifanye douching. Douching inavuruga usawa wa bakteria katika uke wako, na hivyo kufanya maambukizi ya bakiteria wabaya kuingia na kuenea kwa haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *